Ilikuwa mchezo mkali katika uwanja wa Lugalo Veteran zilipokutana timu ambazo zinaelekea kuwa ni wapinzani wa muda mrefu. Mara ya mwisho zilipokutana katika uwanja wa Nyumban wa Survey Veteran, timu ya Lugalo ilishinda wa goli 3-2 na mara hii ilijaribu kutaka kuendeleza uteja lkn mchezo ulikuwa mgumu kwao baada ya kujikuta wakilazimisha sare.
Ilikuwa ni timu ya Lugalo iliyoanza kupata goli kipindi cha kwanza lakini iliwachukua dakika 15 tu Survey Veteran kusawazisha kupitia adhabu ndogo iliyopigwa na Beki hatari Ahmed Shaweji baada ya winga wao hatari Musa Siwiti kufanyiwa madhambi mita 20 toka langoni mwa Lugalo veterans.
Timu zilienda mapumziko zikiwa sare ya goli moja kwa moja. Lugalo walipata goli la pili na Survey kusawazisha baadae kupitia kona mujarabu ilipigwa na winga hatari Musa Siwiti na kumkuta Ahmad Shaweji alioukwamisha mpira wavuni.
Baadae timu zote zilifanya mabadiliko na kufanikiwa kupata magoli. Hadi mwisho wa mchezo SVSC 3 na Lugalo Veteran 3.
0 comments:
Post a Comment