Saturday, 2 January 2016

KATIKA KUELEKEA SHEREHE ZA MWAKA MPYA. TIMU SULEMANI YAIFUNGA TIMU SHABANI GOLI 3-1


Timu Shabani kabla ya mchezo kuanza
Survey veterans katika kuukaribisha mwaka mpya 2016. walicheza mechi ya kirafiki kati yao ambapo Mwalimu alipanga timu mbili ambazo ziliitwa. "Team Sulemani" na "Team Shabani. " ambao Bw. Sulemani ni Katibu Mkuu wa SVSC na Bw. Shabani ni Kaimu Katibu.Mchezo ulianza kwa kila timu kujilinda na kucheza kwa taadhari. Ilikuwa timu Sulemani iliyoanza kupata goli kupitia mshambuliji wao Aaron Nyanda baada ya kupata pasi akiwa katika eneo la kuotea na mabeki wa timu Shabani kumuacha wakizani ameotea. Baada ya muda baadae timu Sulemani walipata goli la pili kupitia kiungo wao hatari Abdala Kassimu.

Hadi timu zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 2-0. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu ikiwa imefanya mabadiliko. iliwachukua muda mfupi kupata goli kwa njia ya penati lililofungwa na Moses baada ya beki wa Timu Sulemani kumchezea rafu kwenye eneo la hatari.

Dakika 20 kabla mpira kumalizika Timu Sulemani iliongeza goli la tatu kupitia mshambuluaji wao Moses. Hadi mpira unaisha timu Suleimani walishinda goli 3-1.

Katika mchezo huo refa alichangia kwa kiasi kikubwa kwa timu Shabani kufungwa baada ya kuonesha upendeleo wa wazi kabisa. Na hata timu Sulemani ilipopata goli la pili alionekana kushangilia kisirisiri. Hii inashauriwa wakati mwingine achaguliwe refa ambaye hana upande katika timu zinazopambana.
Timu Sulemsni kabla ya mchezo kuanza.

0 comments:

Post a Comment