Wednesday, 16 March 2016

BOKO BEACH VETERANS YALALA KATIKA UWANJA WAKE WA NYUMBANI

BOKO  BEACH VETERANS YALALA KATIKA UWANJA WAKE WA NYUMBANI


Timu ya BBV ilijikuta katika wakati mgumu ilipokutana na kichapo cha bao 4-2 dhidi ya Survey Veterans katika uwanja wake wa nyumbani. Ikiwa ya kwanza kupata kupitia adhabu ndogo ilipigwa kiufundi na kumgonga mchezaji wao mmoja na mpira kuingia golini na kuhesabu goli la kuongoza.Iliwachukua dk 15 SVSC kusawazisha kupitia kwa Athumani Kione baada ya kuwapiga chenga mabeki wa BBV. Magoli mengine yalifungwa na Benson Hagai kupitia Kros mujarabu iliyopigwa na Benjamin Magadula. Magoli mengine yalifungwa na Hassan Musa
Baadhi ya wachezaji wa SVSC wakipasha misuri moto kabla kuingia uwanjani

0 comments:

Post a Comment