Sunday, 22 December 2019

MATUKIO YA PICHA KWENYE HARUSI YA EMMANUEL MWANDUMBYA

...

GOLIKIPA WA SURVEY VETERANS AFUNGA NDOA

Golikipa hatari wa SVSC Bw. Emmanuel Mwandumbya ameachana na ukapera baada ya kufunga ndoa takatifu. ...

Thursday, 19 December 2019

BOKO BEACH VETERANS YAENDELEZA UTEJA KWA SURVEY VETERANS

Mara ya pili sasa Boko Veterans inaifunga SVSC. mara ya kwanza ilikuwa magoli 7-2 na mara hii ni 4-3. Magoli ya SVSC yalifungwa na Mwinyi Mwiny magoli mawili na goli la tatu lilifungwa na Sha Pelee Timu ikifanya Maandalizi kabla ya mechi katika uwanja wa Boko Beach Veteran...

Wednesday, 20 November 2019

SURVEY VETERANS BINGWA BONANZA LA WANATAALUMA WA ARDHI

Mratibu wa Bonanza la wanataaluma SV T. Bilauri akikabidhi zawadi kwa mshindi wa wanza Kaptain wa Survey Veterans  Mohamed Adam (Zengwe) baada ya mchezo kumalizika na kuwafunga Surveyor wanafunzi kwa goli 4-1. Timu ya Survey Veterans imeibuka mshindi katika bonanza lililoandaliwa na wapima Ardhi (Surveyors) lilifanyika katika uwanja wa Chuo cha Ardhi Dar es salaam. Golikipa hatari wa SVSC  Emmanuel Mwandumbya  kushoto na Kaptain ...

Tuesday, 15 October 2019

TANGA: MATUKIO YA NJE YA UWANJA

Pamoja na michezo ya Bonanza timu ilifurahi pamoja kama matukio ya picha yanavyoonesha... Madam Datah Daudi akiwaandalia chakula wachezaji baada ya mchezo kumalizika. ...

BONANZA TANGA: ARUSHA ALL STAR YALALA KWA 3-1 MBELE YA SURVEY VETERANS

Mchezo wa pili dhidi ya Arusha All Star walikubali kichapo cha magoli 3-1 Magoli yaifungwa na Kelvin, Ngasa na Sisse. Nahodha wa Survey Veterans Peter Ngassa akimiliki mpira na mchezaji wa Arusha all Star akifuatia kwa karibu.. Arusha ililala kwa magoli 3-1. ...

BONANZA TANGA: SVSC YALAZWA 2-1 NA KOROGWE VETERABS

Mvua kubwa....Hivi ndivyo ilivyokuwa... Kiungo hatari na Naodha wa timu ya SVSC Peter Ngassa akimsaidia Kelvin Haule mwenye  mpira katika mechi ilikuwa iichezwa kwenye uwanja uliojaa maji. Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha mkoani Tanga ilisababisha uwanja kuwa katika hali mbaya na kupelekea SVSC kufungwa magoli 2-1 kwa Tabu sanaaaa Kelvin haule  Mwenye jezi namba 31 wa SVSC akiwa amekusanya kijiji kuelekea golini kwao ....Gooooooool....

SURVEY VETERANS ZIARANI TANGA

Timu ya SVSC imeondoka leo kuelekea jijini Tanga. Pamoja na mambo mengine itashiriki Bonanza liliandaliwa na Timu Mwenyeji ambapo timu kama Moro Veterans, Tanga Veterans ,Kitambi noma Veterans na Timu zingine zinashiriki katika bonanza hilo. ...