Wednesday, 12 August 2015

SURVEY VETERANS YANYA ZIARA YA MICHEZO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO

SURVEY VETERANS YANYA ZIARA YA MICHEZO YA NANE NANE MKOANI MOROGORO

Kikosi cha maangamizi kikiwa katika jezi ya ushindi. Mara nyingi timu imekuwa ikipata matokeo mazuri ikiwa na jezi hii ukilinganisha na jezi za rangi nyingine...

Timu maarufu na kongwe ya SVSC kutoka jijini Dar es salaam ilishiriki bonanza la nane nane lililofanyika mkoani morogoro kwa mafanikio makubwa. Timu ya SVSC iliweza kuilaza timu ngumu ya Morogoro Veterans kwa magoli 2-1 katika mchozo wake wa pili.
Ilikuwa timu ya Morogoro iliyokuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza baada ya kuipenya ngome ya SVSC na kupata goli la kuongoza..
Hadi mapumziko timu ya Moro Veterans ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0. 
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya SVSC kushambulia kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha kwa mkwaju wa penati
iliyopigwa na Kiungo hatari wa SVSC Katibu mkuu Bw. Suleiman Mgaya baada ya krosi nzuri iliyopigwa na Steven Nyenge kumgusa mkononi beki wa timu ya Morogoro Veterans na mwamuzi kuamuru ipigwe penati.

Goli la ushindi liliwekwa kimiani na Kiungo hatari Steven Nyenge (stevovo) akiunganisha krosi nzuri iliyopigwa na winga wa kushoto Said Mahoka. Hadi mpira unaisha SVSC iliibuka na ushindi wa goli 2-1.

0 comments:

Post a Comment