SVSC YATOKA SARE NA MZINGA VETERANS KATIKA BONANZA LA NANE NANE MKOANI MOROGORO
Timu ngumu ya SVSC ilitoka sare ya goli 1-1 na timu ya Jeshi ya Mzinga veterans katika michuano ya nane nane iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwele mkoani morogoro. Timu ya Mzinga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli baada ya mabeki wa SVSC kumuacha mshambuliaji wa Mzinga wakizania ameotea. Hadi tunaenda mapumziko timu ya mzinga ilikuwa mbele kwa goli lao hilo.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya SVSC kushambulia kwa nguvu na kufanikiwa kupata penati baada winga wake hatari Capt Ngasa kuangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati. Penati nzuri ya kiufundi iliyopigwa na Katibu mkuu Suleiman Mgaya ilimuacha golikipa wa Mzinga akiruka kushoto na mpira kwenda kulia. Hadi mpira unaisha timu ziligawana point moja moja.
0 comments:
Post a Comment