Tuesday, 22 March 2016

BOKO INTERNATIONAL VETERANS YAPIGWA BAO 4-1 NA SURVEY VETERANS

BOKO INTERNATIONAL VETERANS YAPIGWA BAO 4-1 NA SURVEY VETERANS

Katika maandalizi kuelekea michezo ya Pasaka,timu za ukanda wa Boko zimekuwa na bahati mbaya sana pale zilipokutana na Miamba ya timu za Veterans Mkoa wa Dar es salaam timu y Survey Veterans yenye maskani yake maeneo ya Survey Dar es salaam.Baada ya Boko Beach Veterans kupigwa magoli 4-2 katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa zamu ya Boko International kupigwa magoli 4-1 katika uwanja wa Survery Veterans. Pia siku ya Ijumaa kuu timu ya SVSC itafanya mazoezi katika uwanja wa JK Kidongo chekundu Dar es salaam kuanzia saa sita mchana kwa hiyo wananchi na wapenzi wa mpira wa miguu wa mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani mnakaribishwa kuja kuwaona wakali wa Timu za Veterans mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya jirani.

0 comments:

Post a Comment