Saturday, 26 March 2016

SURVEY VETERANS YAPOKEA UGENI KUTOKA ZANZIBAR

SURVEY VETERANS YAPOKEA UGENI KUTOKA ZANZIBAR

Timu ya wazee Sports Club kutoka Visiwa vya  Unguja na  Pemba, wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya michezo ya pasaka. Timu hii ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hii iliingia jijini Dar es salaa alhamisi na kupokelewa na wenyeji wao SVSC. Jana tarehe 25/03/2016 walicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tanzania Star na kufungwa magoli 4-3 katika viwanja vya Liders Club. leo tarehe 26/03/2016 wanacheza mchezo wao wa pili na timu ya Boko Beach Veterans katika uwanja wa Jeshi Kunduchi. kwa hiyo wapenzi na wanachama wa timu hizi mbili na wengine tuungane na wageni wetu kwenda kuangalia mchezo wao kabla ya mechi ya kuhitimisha michezo hii, Mechi hii ambayo itafanyika katika uwanja mpya wa Jakaya Kikwete Sports Park kidongo chekundu Siku ya Pasaka. Kutakuwa na michezo miwili , Mchezo wa kwanza utawakutanisha wazee wa timu zote mbili kabla ya mechi ya Maveterans wa timu zote mbili.

MATUKIO YA PICHA YA WAZEE WAKIWA DAR
Wazee Sports Club wakipata chakula cha mchana Makao makuu ya Club ya Survey Veterans  Etina Bar & Restaurant




Mfadhili mkuun wa timu ya Wazee Sports Giga akipata msosi



0 comments:

Post a Comment