Wednesday, 3 April 2019

TIMU YA SVSC YAFUNGWA NA TIMUYA BOKO BEACH VETERANS


Kikosi cha Survey Veterans kutoka kulia walioinama : Paschal Fumbuka, Emmanuel Mwandumbya, Michael Simbaulanga, John Mbitu, Pruce Helman, Peter Simon, Richard Mbunda na Malongo Salvatory. waliosimama kutoka kulia ni Hemedy ,Maulidi, Japhet Tibenda, Geofrey Nyigu, Dominic Mbwete, Hamad Shaweji, Kelvin, Mwalimu Bomba na Siasa.
SVSC ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kukutana na kipigo cha goli 7-1kutoka kwa Boko Beach Veterans. Ikiwa na vijana wenye nguvu na kasi kubwa iliwachukua dk 12 kupata goli la kuongoza baada ya mchezo kuanza. Hadi tunaenda mapumziko SVSC ilikuwa imefungwa magoli 4-0. Goli la kufutia machozi lilifungwa na Peter Mweta kwa mkwaju wa penati baada ya Kelvin kufanyiwa madhambi na beki wa BBV. hadi mpira unamalizika BBV ilishinda magoli 7-1
Peter Mweta akifuatilia mchezo


Peter Simon na Richard Mbunda wakifuatilia mchezo


....Haikuwa rahisi. Richard Mbunda akiwa amesukumwa na baki baada ya kupiga krosi ambayo haikuzaa matunda langoni mwa BBV

Hapa hupiti.....Hemed wa SVSC akijaribu kumtoka beki wa BBV katika mchezo wa kirafiki ambapo BBV ilishinda mchezo huo












0 comments:

Post a Comment