BOMBA DAY ,BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY,
Hivi ndivyo ilikuwa ikitamkika baada ya wazo zuri lililotolewa na mmoja wa wanachama wa SVSC katika kutambua umuhimu na utayari wa kuitumikia timu ambao Bw, Ramadhani Bomba ameuonesha katika kuitumikia timu toka imeanzishwa kama mwl wa timu,
Wazo lilitimia pale wanachama kwa pamoja waliamua kutoa michango yao ili kufanikisha shughuli hii. Tarehe 29/08/2015 ilikuwa siku muhimu katika Timu ya SVSC baada ya kuadhimisha siku hii pale ambapo Mwalimu Bomba kwa Kushirikiana na Capt Mohmed Adam (Zengwe) walipochagua timu miongoni mwa wanachama wa SVSC ambapo Timu y mwalimu iliitwa (Team Bomba) na Timu nyingine iliitwa (Team Zengwe).
Wachezaji wa Timu Bomba walikuwa kama wafuatao...
- Noel (kipa)
- Joseph Mwasenga
- Rasul Ahmed (Dkt)
- James Kabambo
- Osca Mwambungu
- Charles Antipass
- Hagai Benson
- Mahoka Said
- Athuman Kione
- Bilauli
- Juma Massawe
- Ally Mgaya
- Mbunda Richard
- Musa Siwiti
- Sengo Arbat
- Idd Ngaoneka
- Ally Mgaya
- Alfa
- Edwin
- Ngassa Peter
- John MBitu
- Moses
- Feyi
na Timu Zengwe wachezaji waliochaguliwa walikuwa kama wafuatao,
- Ramadhani Njuma (kipa)
- Said
- Hemed Salum
- Mohamed Adam
- Van Bomel
- Gaga Hamisi
- Frank Gaspar
- Hassan Hassan
- Mzee Halifa
- Suleiman Mgaya
- Carlos Mlinda
- Innocent
- Shabani K
- Maulasa
- Kipese Peter
- Luku
Mchezo ulianza kila timu ikicheza kwa taadhari lakini hadi mapumziko timu zote mbili hazikufungana. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambulia kwa zamu, Ilikuwa Timu Bomba iliyoanza kupata goli kupitia kwa Moses na baadae Sengo Arbart aliongeza la pili. Timu Zengwe, walianza Zengwe kwa kufanya mabadiliko.
Iliwachukua dakika 10 kupata goli la kwanza kupitia kwa Innocent Lyimo aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa. Alikuwa Innocent Lyimo tena aliye ipatiagoli la kuongoza Timu ya Zengwe baada ya kuupiga mpira golini huku golikipa akiwa hayupo. Hadi mwisho wa Mchezo Timu Zengwe ilishinda kwa magoli 3-2.
0 comments:
Post a Comment