Monday, 17 December 2018

MATUKIO KATIKA PICHA KABLA NA BAADA YA MCHEZO WA ULINZI VETERANS vs SVSC

Timu ya SVSC wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mchezo kuanza. Captain Peter Ngasaa kushoto  wakijadiliana nani wa kuanza mpira katikati ni Dr. Tiboroa ambaye alikuwa refaree wa mchezo. Vidume vilivyoshereshea mchezo huo wakimsikiliza msemaji wa timu ya upinzani baada ya mchezo kumalizika. Ushindi raha....Baada ya ushindi wa mchezo wa leo. Bw. Frank Gaspar akijipongeza na Castle light baridiiii.... Duh........

ILIKUWA ZAMU YA ULINZI VETERANS

Kikosi cha Ulinzi veterans kabla ya mchezo kuanza Timu changa ya Ulinzi Veterans inayoundwa na maofsa wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania walijikuta katika wakati mgumu katika uwanja wao wa nyumbani Lugalo pale walipokubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka timu kongwe ya Survey Veterans. Pasi mujarabu kutoka kwa Chacha Kibago ilimkuta winga hatari Musa Siwiti na kuukwamisha wavuni kutengeneza goli la kwanza na goli la pili lilifungwa na Albert...

Friday, 2 November 2018

MAPINGA VETERANS YAKIONA CHA MOTO MBELE YA SURVEY VETERANS

Mapinga Veterans walijikuta katika wakati mgumu pale walipokubali kipigo cha magoli 4-1 mbele ya Timu ngumu ya Survey Veterans katika uwanja wa chuo kikuu Ardhi. Iliwachukua dk 15 timu ya SVSC kupata magoli mawili ya kuongoza kufuatia pasi nzuri za winga wake hatari Musa Siwiti ambazo zilimfikia Dulla na kuzikwamisha wavuni. Hadi mpira unamalizika SVSC 4 na Mapinga Veterans bao 1. ...

MAPINGA VETERANS YALALA 4-1 MBELE YA SURVEY VETERANS

Wachezaji wa SVSC wakimsikiliza mwalimu hayupo pichana kabla ya mchezo kuanza Pasi mbili matata kutoka kwa winga hatari, winga wa kuingia nazo Musa Siwiti zilizounganishwa na kiungo Abdallah ziliwafanya Survey Veterans kuongoza kwa magoli mawili ya dakika 15 za kwanza magoli mengine mawili yalifungwa na Edwin Ekingo ambapo aliunganisha kross  kwa kisigino ya mshambuliaji wa SVSC .Hadi mchezo unamalizika SVSC $- na Mapinga Veterans 1 ...

Friday, 28 September 2018

SHEREHE YA MCHEZO YA SVSC vs BBV ILIISHIA HIVI.......

Baada ya mchezo kumalizika katika uwanja wa BBV sherehe iliendelea katika ukumbi wa Maendeleo Bar wanaoonekana kwenye picha ni wachezaji mchanganyiko wageni na wenyeji. Supu ililiwa kama kawaida pamoja na vinywaji laini..... Kama kawaida vinywaji vigumu vilikwepo na wachezaji waliendelea kufurahi kwa pamoja.... David Kiganga kushoto na Idd Ngaoneka wakiendelea na supu huku viburudisho vikionekana kwa mbalaaaali...vikileta maji ya kunawa...

KUELEKEA MCHEZO WA SVSC vs BBV

Kabla ya mchezo kuanza timu ilianza kufanya mazoezi madogo madogo katika uwanja wa Boko Veterans. kutoka kulia ni Suleiman Mgaya, David Kiganga, James Kabambo, Golikipa na John Mbitu wakipasha misuri moto kabla ya mchezo kuanza. Kundi lingine likifanya mazoezi kutoka kushoto ni James Kabambo, Salum Mvule, Dkt Mwinyi Omary,Dkt Mbunda na Beki hatari Peter ndossa Peter ndosa kushoto, Bruce Helman katikati na Michael wakipasha misuri kabla...