Tuesday, 23 April 2019

SURVEY VETERANS MABINGWA MARA NNE MFULULIZO MICHUANO YA PASAKA ZANZIBAR 2019


Timu ya Survey Veterans imewafunga timu ya Wazee Sports Club ya Zanzibar goli 1-0 na kutawazwa kuwa mabingwa mara nne mfululizo. Goli lilifungwa na Kelvin haule kwa shuti kali lilimuacha golikipa wa wazee sports na kutinga wavuni. SVSC walikuwa wapate goli la pili lakini refa aliikataa penati aliyochezewa Kelvin na beki wa Wazee sports. Hadi mwisho wa mchezo SVSC ilishinda goli 1-0.

Kelvin Haule akimwangalia Kipa kabla kupiga mpira ambao ulizaa goli.

Kelvin akishangilia goli huku Captain Peter Ngasa akimfuatia kwa nyuma.


Malongo S. akikosa goli la wazi kabisa baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Wazee Sports.

Kiungo muongomuongo akitoa pasi kwa winga ya kulia Frank gaspar hayuko pichani.....

Kaptain Peter Ngasa akipokea Kikombe cha ubingwa kutopka kwa mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mjini Maghalibi


Mwenyekiti SVSC Bw. John Mbitu akipokea mkono wa shukrani kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghalibi kabla ya kulikabidhi kombe kwa Captain wa timu ya SVSC

0 comments:

Post a Comment