Saturday, 8 June 2019

TIMU ZENGWE YAILAZA TIMU BOMBA MAGOLI 5-2

Kikosi cha timu Zengwe kutoka kushoto waliochuchuma ni Samson Mwakei, Ramadhani, Musa Siwiti, Kasimu Ramia, Sparon Musa, Salum Mvule, Samweli Mbaga (golikipa), Mwandumbya, Michael simbaulanga, Hamis Gaga, Juma Ntalika (Chinga) na Frank Gasper. waliosimama kutoka kulia ni Chacha kibago, Ahmed shaweji, Emanuel Ekingo, Abdalla Kasim, Joseph Mtoimbamba, Ramadhani hamis, David Kiganga, Weston Kipangura, Kelvin Haule, Innocent Kuzengwa, Mwinyi Omary na Siasa.

Kama ilivyo ada inapofika sikukuu ya Idd pili. Timu ya Survey Veterans huadhimisha kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu zinazounda Umoja huu ambayo ni Timu ya Mwl Bomba na Timu ya Mwl Msaidizi Adam Zengwe. kwa mwaka huu Timu bomba ilifungwa magili matano kwa moja.




Winga hatari, winga wa kuingia nazo…… Musa Siwiti akitimiza majukumu yake.





……….Hakuna goli hapa….. Golikipa hatari Mbaga akiokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Benson Hagai ambao haukuzaa matunda…..

……..GOOOOOOOOHHHHHHHHH...…….. Kelvin Haule goli la pili baada ya kupiga faul iliyosababishwa na beki wa timu Bomba Idd Kaonenka baada ya kumchezea madhambi winga hatari Musa siwiti

…….Wengine walikuwa watazamaji tu  Mwenyekiti SVSC alicheza kwa dakika 15 tu akatolewa nje na timu yake baada ya kuonekana alikuwa anadhurura tu uwanjani.

>>>>>Hapa hupiti…. Hamad Shaweji akimdhibiti Peter Simon (Kitop) asilete madhara huku bilauri akimlinda kwa mbali

>>>>>Bunyabunya nao walikwepo japo hawakuwa na mdhara kabisa kwa timu pinzani

Mkwaju wa Weston Kipangule mwenye soksi za njano ulipanguliwa na golikipa wa timu Bomba

…...Hapa upiti Idd Ngaoneka akimkimbiza David Kiganga huku Frank Gaspar akimsaidia kwa nyuma.

Kelvin Haule akifunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi kutoka kwa winga hatari Musa Siwiti hayuko pichani huku beki wa Timu Bomba joseph Mwasenga akiangalia kwa mbali.

0 comments:

Post a Comment