Sunday, 21 December 2014

SALAMU ZA KRISTIMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA KWA MWENYEKITI SVSC

KWA WANACHAMA WOTE WA SVSC MUWE NA SIKUKUU NJEMA AMANI NA UPENDO UTAWALE KUANZIA KWENYE FAMILIA ZENU MPAKA KWA JAMII, JITATHIMINI UMEFANYA NINI KWA MWAKA HUU NA UJIPANGE KWA MALENGO YA MWAKA UJAO. Merry Christimas and Happy New Year 2015,  SVSC idumu!!  Peter Mweta Mwenyeki...

KWA MARA YA KWANZA SVSC IMEFUNGWA 3-2 NA WATOTO WA AZAM JUICE!

Toka mwaka huu umeanza na unaelekea mwisho Timu ya Azam Juice imekuwa ya kwanza kuifunga SVSC kwa taabu timu ya SVSC magoli 3-2 katika uwanja wake wa nyumbamni. Azam Juice ikichezesha vijana tupu ilitangulia kwa goli 2 kabla ya striker hatari wa SVSC Mbunga kuipatia timu yake bao la kwanza. Hadi tunaenda mapumziko magoli yalikuwa 2-1. Baada ya timu zote kurejea kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko kadhaa na walikuwa ni Azam waliotoka na ushindi baada ya mpira kumalizi...

Monday, 8 December 2014

HARUSI YA BW. JAMES MAPEPELE (SHUKURU) YAFANA

 Picha juu na chini inamuonesha Bw. Harusi James Mapepele (Shukuru)...

Monday, 1 December 2014

MASHINDANO YA SHIMMUTA TANGA 2014 YAMALIZIKA

Mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya umma na Makampuni binafsi Tanzania ( SHIMMUTA)yalimalizika tarehe 30/11/2014 mkoani Tanga kwa timu ya Mikopo kuchukua ubingwa wa Mpira wa miguu, Timu ya TBCkutwaa bingwa wa Mpira wa pete na Chuo kikuu ardhi kutwaa ubingwa wa mpira wa kikapu Baadhi ya wanachama na wachezaji wa SVSC walishiriki mashindano hayo kutokea katika taasisi zao wanazofanyia kazi. Majina ya Wachezaji wa SVSC walioshiriki (SHIMMUTA) na  taasisi/makampuni wanakofanyia kazi. kwenye mabano Frank Gaspar, Musa Siwiti, Dr. Kibasa, Benson...

Sunday, 16 November 2014

TANZIA

Mwenyekiti wa Survey Veterans Sports Club anasikitika kutangaza kifo cha mama mzazi  wa Mwanachama mwenzetu Bw Dulla kilichotokea  Jumatano tarehe 12/11/2014 Huko Mwanza.Bw. Dula amesafiri kwenda Mwanza kwa ajili ya msiba huo. Kama ilivyo ada na utaratibu wetu tumuombee na kumsaidia katika hali na mali katika kufanikisha msiba huu. Mungu ailaze mahari pema peponi Roho ya marehemu mama yetu mpendwa  Amen Peter Mweta Mwenyekiti S...

TANZIA

Mwenyekiti wa Survey Veterans Sports Club anasikitika kutangaza kifo cha mama mzazi  wa katibu mkuu SVSC Bw. Suleiman Mgaya na Mjumbe kamati ya ufundi Bw. ally Mgaya. kilichotokea  Alhamisi tarehe 13/11/2014 hapa jijini Dar es salaam na kusafirishwa kwenda kijijini kwao Kibindu wilaya  ya Bagamoyo kwa mazishi ambayo yalifanyika tarehe 14/11/2014 Mungu ailaze mahari pema peponi Roho ya marehemu mama yetu mpendwa  Amen Peter Mweta Mwenyekiti S...

Monday, 27 October 2014

SHUKRANI KUTOKA KWA MWENYEKITI WA SURVEY VETERANS

Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta anapenda kutoa shukrani za dhati kwa wapenzi na wanachama wa SVSC waliofanikisha safari hii muhimu na ya kiistoria. Pia anapenda shukrani ziwaendee hata wale ambao hawakubahatika kwenda kwa sababu mbalimbali na kuwaomba wanachama kudumisha upendo na umoja huu.... (alisema) "Nimefarijika sana kufanikisha safari hii kwani tulikuwa tunaisubiri toka mwezi Augost na sasa imekamilika......" Kundi la mwisho la wachezaji na wanachama wa SVSC lilirejea Dar es salaam salama kutokea Mwanza jana jioni kwa ndege ya shirika...

Sunday, 26 October 2014

SURVEY VETERAN YAREJEA DAR

Timu ya Survey Veterans imerejea leo mapema ikitokea Ziarani Mwanza ambapo katika mechi yake na wenyeji Mwanza Starehe Veterans iliwafunga goli 4-2 Picha za matukio: Picha juu na chini kikosi kilichoiangamiza Mwanza Starehe Veterans Captain Peter Ngassa wa pili kutoka kushoto alifunga magoli mawili.....

Friday, 24 October 2014

SURVEY VETERANS YAILAZA MWANZA VETERANS 4-2 KATIKA ZIARA YAKE JIJINI MWANZA

Timu ya Survey Veterans kutoka Dar e salaam, imeilaza timu ya Mwanza StareheVeterans kwa magoli 4-2 katika uwanja wa CCM Kilumba Jijini Mwanza.Magoli ya Survey VeteransYalifungwa na Peter Ngasa, magoli 2,Innocent Lyimo na  Said Omary kwa mkwaju wa penati.Magoli ya wenyeji yalifungwa na Juma Amir Maftah na Mbuyi Yondani. Kikosi kilichoizamisha Mwanza Starehe Veterans kiliongozwa na Golikipa  Kilibe, fullbacks James Kabambo na Dr Rasul Ahmed,...

SURVEY VETERANS YATUA SALAMA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA

BAADHI YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA svsc KATIKA PICHA YA PAMOJA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA...  .....Baadhi ya wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza....  Katibu Mkuu wa survey Veterans na Mjumbe kamati ndogo ya Nidhamu wakiwa uwanja wa ndege wa Mwanza... baada ya kuwasili wakitokea Dar es salaam...

KUNDI LA MWISHO LA SURVEY VETERANS LAPANDA NGEGE KUELEKEA MWANZA

AWAMU YA MWISHO YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA svsc WAMEONDOKA LEO SAA NNE MJINI DAR SALAAM KUELEKEA MWANZA KWA ZIARA YA KIMICHEZO Baadhi ya wachezaji wakiwa uwanja wa ndege wa JKNIA tayari kwa safari  Bw. Ngasamiaku akipata news katika sehemu ya kusubiri tayari kwa safari,......  Mwenyekiti mstaafu Bw. Bakuza M.. pamoja na wanachama wengine katika waiting longe tayari kwa safari  Stevovo", Cobi tayari kuelekea...

Thursday, 23 October 2014

BAADHI YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA SVSC WAWASILI UWANJA WA NDEGE MWANZA

 Carlos Mlinda namuona kwa mbali akiwa ameshika "begi lake la matairi" akiwa wa kwanza kuteremka kwenye ndege...  M/Katibu naye akiwa ameshikilia begi lake kwa makini "kuogopa wezi" Bw. Innocent baada ya kuteremka "kwenye mwewe" Mhazini Msaidizi akifurahia jambo uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kuteremka...

TIMU YA SURVEY VETERANS ZIARANI MWANZA

TIMU YA SURVEY VETERANS IMEWASILI LEO ASUBUHI JIJINI MWANZA KWA ZIARA YA MICHEZO YA KIRAFIKI. TIMU MWENYEJI NI  MWANZA STAREHE VETERANS JIONI YA LEO  ITAKIPIGA NA TIMU YA....... Juu na chini ni picha za Wachezaji na wanachama wa SVSC wakiwa uwanja wa ndege wa JNIA tayari kwa safari ya Mwanza na ndege ya Fastjet  Baada ya Ku "Chech in" Katibu wa SVSC Bw. Suleiman Mgaya , Mjumbe kamati ndogo ya Nidhamu Bw. Frank...

Wednesday, 22 October 2014

LUGALO VETERAN YALAZIMISHA SARE NA SURVEY VETERANS

Timu ya Lugalo veterans ilipunguza uteja pale ilipolazimisha sare ya goli 2-2 na timu ngumu ya Survey Veterans mechi iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani wa SVSC.Timu ya Survey Veterans imekuwa kinara kwa timu nyingi za veterans za mkoa wa dar esalaam na mikoanipia. Angalia picha na matukio ya mechi hiyo... Timu ya Lugalo veterans ambayo ilitoka sare ya magoli 2-2 na Timu ya Survey veterans. ...

ETINA BAR & RESTAURANT YANDAA PATI KWA AJILI YA KUWAPONGEZA SURVEY VETERANS

Mkurugenzi mtendaji wa Etina bar & Restaurant Bi Catherine Swai amewapongeza wapenzi na wachezaji wa timu ya Survey Veterans kwa ushindi wao walioupata katika Bonanza la Serengeti fiesta lililofanyika katika viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe. Pia Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta alimshukuru kwa kutambua mchango wao katika kulitangaza jina la Bar hiyo.  Mwenyekiti Bw. Peter Mweta aliwaongoza wachezaji na wanachama katika zoezi la kukata...